Polisi wa Uganda, inawashikilia watu wengine watano huku ikigundua vilipuzi vingine vitano katika eneo lililo karibu na mji Mkuu wa nchi hiyo Kampala, katika njama ya kulipua mabomu inayohusishwa na kundi la waasi wa Kiislamu, Allied Democratic Forces – ADF.

Vikosi hivyo, vyenye makao yake katika misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC, vimeungana na vuguvugu la wanamgambo wa Islamic State na kwa miaka mingi wameshambulia raia na maeneo ya kijeshi huko DRC na Uganda.

Mshukiwa wa kwanza, alikamatwa akiwa na bomu kwenye begi nje ya Kanisa moja lililokuwa likiendelea na Ibada siku ya Jumapili Septemba 2, 2023 na kusababisha msako ambao ulipelekea kukamatwa kwa watu wengine watano na kupatikana kwa vilipuzi vingine vitano.

Taarifa ya Jeshi la Polisi nchini humo imesema, mabomu hayo yaliteguliwa kwa usalama ambayo yalitengenezwa na vitu kadhaa vikiwemo misumari, betri na vifaa vya kulipua vilipatikana baada ya watu hao kutiliwa mashaka na Vyombo vya usalama kwa ushirikiano na wananchi.

Mayele: Huyu Maxi ni moto wa kuotea mbali
Uhaba wa Mafuta: Malisa awatoa hofu wakazi wa Mbeya