Jeshi la Polisi mkoa Morogoro, kitengo cha Dawati la jinsia na watoto Wilaya Malinyi limewataka wananchi kuacha kuvumilia vitendo vya aina yoyote ya kikatili watakavyofanyiwa katika maisha yao ya kila siku.

Rai hiyo imetolewa na Konstebo Herieth wakati akitoa elimu kwa Wanawake waliohudhuria clinic katika Hospitali ya Wilaya ya Malinyi, ambapo amesema vitendo hivyo si sehemu ya maisha yao kwani havikubaliki katika jamii na ni kinyume cha haki za binadamu.

Aidha, amewataka kutoa taarifa zote za vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto, ili watuhumiwa waweze kukamatwa na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Konstebo Herieth, pia aliwahakikishia usiri uliopo katika Jeshi la Polisi kwa yeyote ambaye hatohitaji kujulikana kuwa ametoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto, hasa unaofanywa na ndugu wa karibu.

Jela miaka 30 kwa kosa la kubaka Mtoto
Tanzania kushirikiana na IFAD miradi Sekta ya Kilimo