Mahakama ya Wilaya Kasulu Mkoani Kigoma, imemhukumu kifungo cha miaka 30 Jela Emmanuel Charles(34), pia kulipa fidia ya fedha taslimu Shilingi 300,000 baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa kike (14), mkazi wa Shunguriba.

Akitoa hukumu hiyo Septemba 6, 2023 Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Kasulu, Imakulatha Shuri amesema mahakama imejiriridhisha pasi na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hatimae kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.

Mshitakiwa huyo, ambaye ni Mkulima na mkazi wa Kijiji cha Shunguriba Wilayani Kasulu, anadaiwa kutenda kosa hilo Desemba 25, 2022 katika Kijiji cha Shunguriba Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma na alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Januari 16, 2023.

Hata hivyo, Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wengine wanaojihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa sheria, maadili na ukatili dhidi ya Watoto.

Taifa Stars ikijitega imejitega
Ukatili si sehemu ya Maisha yako - Dawati la jinsia