Beki wa Real Madrid, Dani Carvajal amekiri wachezaji wenzake walidhani Kylian Mbappe aingejunga nao katika dirisha la majira ya kiangazi.

Mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain alihusishwa na Madrid baada ya kugoma kusaini mkataba mpya PSG, lakini alibaki jijini Paris.

Lakini kwa mujibu wa beki huyo, waliona kila dalili kwamba Mfaransa huyo angetua Santiago Bernabeu baada ya kujadili na wenzake.

Carvajal alisema: “Siwezi kudanganya kwamba hatukujadili, lakini wakati tupo katika ziara Marekani maneno mengi yalizungumzwa. Nilidhani angejiunga (Madrid) na nilijua Mbappe angechagua timu yetu.

Baada ya kukosa ziara ya PSG niliamini anatua kwetu, lakini mambo hayakwenda kama tulivyotarajia.”

Mbappe alitatua mzozo na mabosi wake PSG ambao ulidumu muda mrefu bila kupata muafaka kuhusu hatima yake.

Tàarifa zilidai angesaini mkataba mpya PSG utakaodumu hadi 2026 na utajumuisha kipengele kipya kitakachomwezesha kusajiliwa na Madrid siku za usoni.

Mbappe ameanza Ligi Kuu Ufaransa kwa kishindo, kwani katika mechi tatu alizocheza amefunga mabao matano.

Mahakama yatupilia mbali hoja za Wapinzani
Waziri Mkuu ampa Biteko maagizo changamoto bei ya Mafuta