Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itaongeza usalishaji wa mbegu bora za kisasa, ili kuboresha sekta ya kilimo na kuwavutia Vijana kwenye sekta hiyo adimu.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Septemba 7, 2023 kwenye Jukwaa la Mifumo ya Chakula linalofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Marais wa nchi 7 wa Afrika kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula kwa nchi zao.

Aidha, Rais Samia pia amesema Serikali yake itajenga vihenge vya kisasa ili kuhifadhia mazao ya chakula, kama njia ya kuongeza tija katika sekta ya kilimo nchini.

#RaisSamia #KeshoBora #AGRF2023.

Mazao kufikishwa Sokoni, bei ya Mbaazi yapanda
Kila Mkulima kupimiwa afya ya Udongo - Rais Samia