Uongozi wa Klabu Bingwa nchini England ‘Manchester City’, una mpango wa kumpatia ofa mpya staa wake, Erling Haaland ya mshahara wa pauni 600,000 kwa juma.

Imeelezwa kuwa, Man City wanataka kumpa ofa nono Haaland kwa kusaini dili jipya, huku sababu za kufanya hivyo ikiwa ni kuhakikisha staa huyo anashindwa kujiunga na Real Madrid kuanzia msimu ujao au kwenda Saudi Arabia.

Haaland kama atasaini dili hilo jipya na kulipwa pauni 600,000, atakuwa ndiye mchezaji anayelipwa zaidi ndani ya Premier League.

Mshambuliaji huyo alisajiliwa na Man City akitokea Borussia Dortmund msimu uliopita, baada ya kutua hapo amekuwa chachu ya mafanikio ya timu hiyo.

Haaland akiwa na Man City, msimu wake wa kwanza amefanikiwa kutwaa mataji matatu ambayo ni Ligi ya Mabingwa Ulaya, Premier League na Kombe la FA.

Lakini pia staa huyo alikuwa mfungaji bora wa UEFA, Premier League na Ulaya kwa jumla.

38 Wakamatwa wakitorosha Mifugo Nchini
Wachezaji Young Africans wahamasishwa