Uongozi wa Dodoma Jiji umeweka wazi kuwa kwa sasa benchi lao la ufundi linaendelea kuwapa program wachezaji wao wakiwa wanajiandaa kwa michezo ijayo.

Ikumbukwe kuwa Dodoma Jiji wamecheza mechi mbili dhidi ya Coastal Union ambayo walipata ushindi na ile dhidi ya Simba SC ambayo walifungwa mabao 2-0.

Akizungumza mjini Dodoma, Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga alisema: “Hali ya wachezaji kwa ujumla wanaendelea na maandalizi na program ambazo mwalimu anawafundisha ili kuweza kupata alama tatu.

“Ligi ni ngumu sana ukiangalia kila timu imesajili wachezaji wazuri kwa ajili ya kupata ushindi. Tutaendelea kupambana ili kuweza kushinda kila mechi iliyopo mbele yetu.

“Mashabiki waendelee kuwa na sisi malengo yetu ni yale yale ya kufanya vizuri na niwahakikishie tutawapa burudani ya kutosha wajitokeze kwa wingi bila wao sisi hatuwezi”.

Serikali, Wadau wa Afya kuendesha Kampeni chanjo ya Polio
Serikali yakanusha madai GGML 'ku-blacklist' Vijana Nchini