Uongozi wa Coastal Union umesema utahakikisha kuwa unafanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Mpaka sasa kwenye ligi Coastal ipo nafasi ya 10 ikiwa na alama moja baada ya kucheza michezo miwili, ikipoteza mchezo mmoja na kutoa sare moja.

Akizungumza jijini Tanga, Ofisa Habari wa Coastal Union, Abbas E-Sabri amesema kuwa uongozi una malengo makubwa inayofanyia kazi kwa msimu mpya.

“Tuna malengo ya kufanya vizuri kwenye ligi ili kushiriki mashindano ya kimataifa na hilo linatufanya tufikirie kumaliza ndani ya nafasi nne za juu.

“Pia tuna malengo ya kuchukua taji la Azam Sports Federation hilo linawezekana kwa kuwa tuna nia ya kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao.”

Man Utd kinara wa mtumizi ya fedha
Jamie Carragher: Mo Salah ataondoka Liverpool