Manchester United wanasema wanachukulia kwa uzito tuhuma zilizotolewa dhidi ya winga wao Mbrazili, Antony baada ya kutuhumiwa kumfanyia vurugu mpenzi wake wa zamani.

Chombo cha habari cha Brazil UOL kilichapisha madai yaliyotolewa na mpenzi wa zamani wa Antony siku ya Jumatatu.

Polisi mjini Sao Paulo na Greater Manchester wanachunguza madai hayo, ambayo mchezaji huyo ameyakanusha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliondolewa kwenye kikosi cha Brazil baada ya habari za madai hayo kuibuka.

United walisema: “Manchester United inakiri tuhuma zilizotolewa dhidi ya Antony na inabainisha kuwa Polisi wanaendelea na uchunguzi. Inasubiri taarifa zaidi, klabu haitatoa maoni zaidi.

“Kama klabu tunalichukulia suala hili kwa uzito mkubwa, kwa kuzingatia athari za tuhuma hizi na kuripoti baadae kutakuwa na waathirika wa unyanyasaji.”

Antony alisema kwenye mtandao wa kijamii; “Ninaweza kusema kwa utulivu kwamba shutuma hizo ni za uongo na kwamba ushahidi ambao tayari umetolewa na ushahidi mwingine utakaotolewa unaonyesha kwamba sina hatia katika tuhuma zinazotolewa.”

Antony anashutumiwa kwa kumshambulia mpenzi wake wa zamani, Gabriela Cavallin kwa kumpiga kichwa katika chumba cha hoteli ya Manchester mnamo Januari 15. Pia anadai alipigwa ngumi ya kifua, na kusababisha majeraha.

Serikali yakanusha madai GGML 'ku-blacklist' Vijana Nchini
Gamondi amuandaa Skudu kuivaa El Merrikh