Beki wa Kulia wa Simba SC Shomary Salum Kapombe amesema ushiriki wao katika michuano ya African Football League utazidi kuifanya timu hiyo iwe bora zaidi Kimataifa na kama wachezaji wamejiandaa kufanya kweli.

Simba SC imepangwa dhidi ya Al Ahly ya Misri katika mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo mipya, inayoshirikisha pia Esperance (Tunisia), Wydad Casablanca (Morocco), Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Enyimba (Nigeria), TP Mazembe (Congo) na Petro Atletico (Angola).

“Michuano hii ni mikubwa, sio kwa timu hata kwa wachezaji tumeingia katika historia ya kipekee kuanza kuicheza na bahati kubwa Simba SC imeingia ikiwa kati ya klabu nane Afrika, tunaendelea kujipanga maana ushiriki wetu utatufanya kufanya vizuri zaidi katika michuano mingine ambayo timu itashiriki,” amesema

Pia, amesema wachezaji wote wanaufahamu ubora wa Al Ahly na ukubwa wake hivyo ni moja ya kipimo kizuri kwa wachezaji. “Tutaendeleza historia yetu ya Kwa Mkapa hatoki mtu, maana tunajivunia wingi wa mashabiki wetu, tutahakikisha tunapambana kufanya vizuri katika michuano hii,” amesisitiza Kapombe aliyekuwa walipoizamisha Al Ahly kwa bao 1-0 katika mechi za makundi ya Ligi ya Mabingwa 2020-2021 kwa bao lililofungwa na Luis Miquissone ambaye baadae alisajiliwa na klabu hiyo.

Mashabiki wachukulia poa ishu ya Ronaldo
38 Wakamatwa wakitorosha Mifugo Nchini