Mashabiki wa soka duniani hawajashangazwa kufuatia Cristiano Ronaldo kuondolewa katika majina ya wachezaji wanaowania Tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno alikuwemo muda mrefu katika orodha ya wachezaji wanaowania tuzo hizo kwa muda mrefu tangu mwaka 2004.

Hata hivyo, baada ya kupitia kipindi kigumu msimu wa 2022-23, alitimkia Saudi Arabia na kuachana na soka la Ulaya baada ya kuondoka Manchester United.

Licha ya kufunga mabao 26 katika mechi 33 alizochza Al-Nassr, Mreno huyo mwenye umri wa miaka 38 alitemwa katika majina 30 ya awali ya wanaowania Tuzo ya Ballon d’Or.

Licha ya kuwepo katika orodha za Tuzo ya Ballon d’Or tangu mwaka 2003, mashabiki walitoa maoni mbalimbali kupitia mtandao wa kijamii wa X baada ya mwaka huu kutemwa huku wengine wakimponda.

Shabiki wa kwanza akaandika: “Mashabiki wa Ronaldo walimcheka Messi alipotemwa msimu uliopita sasa tuone.”

Shabiki mwingine akaandika “Haijalishi hata kama hayumo amepata mafanikio mengi.” Shabiki wa tatu akasema: “Waandaaji wa tuzo hizo wanamchukia Ronaldo.”

Mwingine Aliandika “Inashangaza tunajua Ronaldo ni bora.”

Orodha hiyo imejumuisha mastaa kama Erling Haaland, Kylian Mbappe na Lionel Messi.

Wanahabari wajengewa uwezo matumizi ya Gesi mbadala
Kapombe: AFL itatuimarisha Kimataifa