Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amesema mshambuliaji wake, Alassane Diao anahitaji muda ili kuwa katika kiwango chake.

Akizungumza Dar es salaam, kocha huyo amesema Diao anahitaji muda kuzoea mazingira lakini pia anahitaji kupewa nafasi ili kuonesha kile alichonacho.

“Diao anahitaji muda kwa sababu hata wachezaji wenzake hawafahamu uchezaji wake, hawamuelewi vizuri, naamini muda sio mrefu watamuelewa na kutupa kile ambacho tunakitarajia kutoka kwake, amesema.

Mchezaji huyo aliyetokea klabu ya US Goree ya Senegal hajaonesha ubora unaotarajiwa na wengi kama ilivyoelezwa wakati akisajiliwa na Azam FC huku akiwa amepewa dakika chache uwanjani katika mechi za hivi karibuni za Azam FC.

Katika mechi mbili za Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho Afrika na za Ngao ya Jami, mchezaji huyo hakupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza zaidi ya kuanzia benchi.

Jamie Carragher: Mo Salah ataondoka Liverpool
Ronaldo: Ushindani wangu na Messi umekwisha