Gwiji wa klabu ya Liverpool, Jamie Carragher anaamini Mohamed Salah ataondoka katika klabu hiyo siku za usoni baada ya dili kubuma katika dirisha la usajili la kiangazi.

Mchambuzi huyo wa Kituo cha Televisheni cha Sky Sports alitoa maoni yake akidai ni suala la muda tu na hatashangaa kama Salah akiondoka katika kipindi cha miezi 12 ijayo.

Akizungumzia kuhusu hatma ya fowadi huyo wa kimataifa wa Misri, Carragher alisema: “Mkataba wake utamalizika kabla ya mashabiki kujua.

“Nadhani hisia za mashabiki wengi wa Liverpool wanadhani Salah atacheza zaidi ya msimu mmoja.

“Kama Liverpool itamuuza Salah itapata pesa ndefu na itasajili mbadala wake siku za usoni, lakini ngumu sana kupata mchezaji wa ubora wake, labda atatokea sijui nafikiri Liverpool ina miezi 12 ya kufikiria mchezaji mwingine ambaye atakuja kuziba pengo lake.”

Salah alizua presha Liverpool ambayo iliweka wazi haina mpango wa kumuuza katika kipindi cha usajili wa kiangazi mwezi uliopita baada ya Al-Ittihad kuweka ofa ndefu.

Taarifa ziliripoti Salah alilazimisha kuondoka Anfield hata hivyo, Liverpool ilisisitiza nyota huyo wa kimataifa Misri hauzwi kwa dau lolote. AI-Httihad ilikuwa na nia ya dhati ya kumsajili Salah na ilitoa ofa zaidi ya Pauni 200 milioni hata hivyo Liverpool ikapiga chini ofa hiyo na kumzia kuondoka.

Coastal Union kufuata nyayo za Singida FG
Kocha Azam FC amkingia kifua Alassane Diao