Takriban watu 14 walifariki na wengine wanne kujeruhiwa baada ya Basi dogo la Abiria maarufu kama Matatu kugongana ana kwa ana na Lori eneo la Ndii lililopo barabara kuu ya Nairobi-Mombasa, karibu na mji wa Voi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Voi, Benastine Shari amesema watu hao 13 walifariki papo hapo, huku wengine wanne wakijeruhiwa vibaya.

“Ninapozungumza na wewe, watu 13 wamethibitishwa kufariki. Bado tunaondoa miili iliyonasa kutoka kwenye mabaki hayo,” amesema Kamanda Shari.

Aidha ameongeza kuwa, “Dereva wa matatu alikuwa katika mwendo kasi. Ajali hiyo ilitokea alipokuwa akijaribu kulipita gari lingine. Matatu hiyo iligongana uso kwa uso na lori na waliofariki ni abiria wote wa matatu.”

Mashabiki Rwanda waisubiri Young Africans
Tetemeko lauwa 300 Morocco