Nyota wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo amelipua bomu kwa mashabiki akidai yeye na Lionel Messi upinzani wao umekwisha baada ya kuondoka Ulaya.
Messi na Ronaldo walishiriki kwenye ligi moja kubwa, La Liga kwa muda mrefu na kwa mafanikio makubwa katika maisha yao ya soka lakini sasa wanakipiga katika ligi tofauti nje ya Ulaya.
Wawili hao walichuana vikali kwenye tuzo 12 za Ballon d’Or ndani ya miaka 13 huku wakipata mafanikio katika ngazi ya klabu na timu za taifa.
Uhamisho wa Ronaldo kwenda Juventus ulimaliza kukutana kwao katika hafla za sherehe za Balon dOr kila msimu tangu mwaka 2019, kabla ya kutimkia Saudi Arabia Januari mwaka huu na baada ya Messi kujiunga na Inter Miami msimu huu, imewafanya mastaa hao kucheza katika mabara mawili tofauti.
Kuondoka kwa Messi na kutimkia Marekani ilionyesha huo ndio mwisho wa upinzani wao, ingawa bado wanachuana vikali katika ngazi ya kimataifa.
Katika mahojiano na waandishi wa habari, Ronaldo alimsifu Messi akidai walikuwa wakiheshimiana kwa muda mrefu licha ya mashabiki kuchochea “Chuki’ Sikuuchukulia ushindani wetu kwa mtazsmo huo, upinzani wetu umeshakufa, watu wanaompenda Ronaldo hawatikiwi kumchukia Messi, tulifanya mambo mengi, tulibadilisha historia ya soka. Tunaheshimika duniani kote, hilo ndilo jambo la msingi,” alisema Ronaldo.