Baada ya kuanza vibaya kwenye michezo yao miwili ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha Mkuu wa kikosi cha Namungo FC, Cedric Kaze ameweka wazi kuwa tayari wameona wapi walikuwa wanakosea na kuahidi kufanya makubwa kwenye michezo yao ijayo.

Kocha huyo kutoka nchini Burundi ameweka wazi kuwa anajivunia namna ambavyo wachezaji wake wamekuwa wakitimiza maelekezo ya Program anazotoa.

Kaze amesema: Nafurahishwa na namna ambavyo tumekuwa na maendeleo mazuri ya Programu za maandalizi ya michezo yetu ijayo hasa kutokana na kuanza ligi kwa kusuasua.

Tumerekebisha makosa yetu na sasa ni muhimu kuendelea na kasi hii kwa ajili ya mechi zijazo kwani ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo.”

Jadon Sancho anajitafuta tena Man Utd
Filippo Inzaghi: Lukaku atatoboa AS Roma