Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu
amesema atatoa maelezo Polisi hii leo Septemba 11, 2023 kama alivyotakiwa kufanya na  Jeshi  hilo katika Kituo cha Polisi Mkoani Arusha.

Lissu aliyasema hayo mbele ya Waandishi wa Habari muda mchache baada ya yeye na wenzake kuachiwa kwa dhamana kufuatia kukamatwa wakituhumiwa  kufanya mikutano isivyo halali na kuwazuia Askari kufanya kazi yao.

Jana, Septemba 10, 2023 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe alisema wanalaani ukamataji, unyanyasaji na usumbufu unaofanywa na Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Dola kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu na Viongozi Waandamizi wa ngazi mbalimbali na  Wanachama.

Mbowe alitoa kauli hiyo baada Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kuthibitisha kumshikilia Lissu na Watu wengine watatu kwa mahojiano kuhusiana na tuhuma za kufanya mikusanyiko isivyohalali na kuwazuia Polisi kutekeleza majukumu yao.

Dola Bil. 4.7 kuendeleza Wataalamu wa TEHAMA
Ndege Nyuki yauwa zaidi ya 40 Sokoni