Mshambualiaji wa Mtibwa Sugar, Abalkassim Suleiman amefichua sababu za kujiunga na timu hiyo msimu huu akiipiga chini ofa ya West Armenia inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo.

Abalkassim amesema timu hiyo ilionyesha nia ya kumsajili, lakini washauri wake baada ya kupitia vipengele vya mkataba aliotumiwa ausaini walishindwana, hivyo kubaki hapa nchini.

“Mkataba walionipa haukuangalia maslahi yangu zaidi isipokuwa uliegemea kwao. Ndio maana tulisumbuana sana baada ya kuona wanachelewa kunipa majibu niliamua kufanya uamuzi mwingine,” amesema.

Abalkassim ameongeza kwa sasa ameelekeza akili na nguvu katika maisha yake mapya ndani ya Mtibwa Sugar huku akiwaahidi mashabiki wa timu hiyo watarajie mazuri msimu huu kutokana na ushirikiano uliopo wa wachezaji na benchi la ufundi.

Nyota huyo aliyefunga mabao manne ya Ligi Kuu Bara msimu uliopita akiwa na Ruvu Shooting iliyoshuka daraja, amejiunga na kikosi hicho huku akitegemewa kutengeneza pacha na mshambuliaji mwenzake, Matteo Anthony.

Diaspora wamlilia Kairuki, waahidi ushirikiano kwa Balozi Khamis
Ajali ya Boti yauwa 26, wengine hawajulikani walipo