Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouf Dabo amewataka washambuliaji wake kuongeza umakini kuzitumia vizuri nafasi nyingi wanazozitengeneza.

Dabo ametoa msisitizo huo baada ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Arta Solar kutoka Djibout uliopigwa Jumamosi (Septemba 09), ambapo amesema tatizo la kushindwa kuzitumia vizuri nafasi kwenye timu yake limekuwa likimsumbua tangu wakiwa kambini Tunisia.

“Ni kweli tunafunga mabao lakini hayana uwiano mzuri na nafasi tunazotengeneza mara nyingi tumekuwa bora kwenye kutengeneza nafasi lakini washambuliaji wameonesha kukosa utulivu na kuzitumia chache kitu ambacho sio kizuri,” amesema Dabo.

Kocha huyo amesema pamoja na changamoto hiyo yeye na wenzake wataendelea kupambana ili kurekebisha tatizo hilo kwenye mechi zijazo za Ligi Kuu na michuano ya Kombe la FA watakayoshiriki baadae. Katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Azam Complex Chamazi, Azam FC ilibuka na ushindi wa mabao 2-1, mabao yakifungwa na Feisal Salum na Prince Dube.

Sare yamchukiza Gareth Southgate
Kramo awasononesha viongozi Simba SC