Polisi Kata wa Kidodi Kilosa Mkoani Morogoro, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Aiden Mufundi, amewataka akina mama kuendelea kuwa imara katika malezi ya watoto, kwa kuwaeleza namna ya kukabili changamoto za ukatili na unyanyasaji kwa kila hatua katika makuzi yao.

Mufundi ameyasema hayo wakati wa utoaji wa elimu kwa akina mama hao wa Kata wa Kidodi iliyopo Wilayani Kilosa mkoani humo na kuongeza kuwa ili kukabili changamoto za matukio ya kiuhalifu ni vyema akima mama hao wakawapa utambuzi watoto wao kwa kila hatua yao ya ukuaji.

Amesema, “tumewaita pamoja na watoto wenu ili wasikie haya tunayowaeleza kwani wa mama mmekuwa na kawaida ya kuogopa kuongea na wototo wenu mkijua kuwa mnajenga kumbe mnabomoa, kuanzia sasa mnapaswa muwe ngangari na mseme nao.”

Aidha, kwa upande wao akina mama hao walionesha kuguswa na elimu hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi yale yote waliyoelezwa na Polisi kata, huku wakiomba elimu hiyo itolewe mara kwa mara kwani itawajengea uwezo wa kuwasimamia watoto wao kimaadili.

Niyonzima aipeleka Young Africans Makundi CAF
Mafunzo huduma za afya kuwanufaisha Wagonjwa wa Moyo