Imefahamika kuwa Kiungo Mshambuliaji ‘Winga’ Jadon Sancho anaweza kupewa nafasi ya kurejea tena kwenye klabu yake ya zamani Borussia Dortmund inayoshiriki Ligi Kuu Ujerumani.

Manchester United, iliulizwa na mabosi wa Dortmund kama wanaweza kumruhusu Sancho kurejea kwa mkopo kwenye klabu yao na dalili zinaonesha kuwa hilo linaweza kutimia.

Sancho na Erik ten Hag wameingia katika mzozo wa kushangaza, kila mmoja akimshutumu mwenzake kwa kutokuwa muwazi kwenye jambo fulani.

Winga huyo alizozana na kocha wake Ten Hag baada ya kupoteza kwa mabao 3-1 Jumapili iliyopita dhidi ya Arsenal.

Ten Hag alifichua kuwa alimuacha nje ya kikosi cha United Sancho kwa sababu ya utendaji wake finyu katika uwanja wa mazoezi.

Hata hivyo Sancho alijibu, akisema hilo si kweli na alikuwa amefanywa Mbuzi wa kafara kwenye kipigo chao na Gunners.

Kwenye mtandao wa kijamii, Sancho aliandika pia: “Sitaruhusu watu kusema mambo ambayo si ya kweli kabisa, nimejitahidi kufanya kwa ubora mazoezi wiki hii.”

Uhusiano kati yao unabaki kuwa mbaya na viongozi wa Dortmund wanafuatilia kwa karibu jinsi hali inavyoendelea katika miezi michache ijayo.

Sancho, ambaye alicheza mechi tatu akitokea benchi kabla ya mechi ya Arsenal, amekuwa hana maisha mazuri United tangu kuwasili kwake kwa Pauni Milioni 73 mwaka 2021.

Alitumia miezi mitatu nje ya kikosi cha kwanza msimu uliopita, akifanya mazoezi peke yake chini ya uangalizi wa kocha huyo Mholanzi.

Robertinho ajivunia washambuliaji wake
Al-Ittihad kuhamishia vurugu Tottenham