Kupitia mafunzo yanayotolewa na UN WOMEN, yamewahamasisha Wanawake wa Wilaya tatu za mkoa wa Pwani kushiriki chaguzi mbalimbali ikiwemo wa Serikali za mitaa na uchaguzi Mkuu wa 2025.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo hayo, Mratibu wa Mafunzo Afisa Maendeleo ya jamii Halmashauri ya Kibaha Mji, Maria Nkangali amezitaja Wilaya zitakazonufaika na Mafunzo hayo kuwa ni Kisarawe, Chalinze na Kibaha Mji.

Amesema, Mafunzo hayo pia yamehusisha makundi mbalimbali wakiwemo Watu wenye ulemavu, wazee wa Mila na Walimu na yamekuja wakati muafaka kutokana na mwitikio mdogo wa Wanawake kushiriki Katika Chaguzi kupata nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa upande wake Mratibu wa Dawati la uwezeshaji Wananchi kiuchumi, Mkaminoela Hangaya amesema Katika majukwaa hayo Wanawake Wengi hawana Elimu ya Biashara, hivyo yatasaidia Wanawake kujikwamua kiuchumi.

Usiri wagubika mkutano wa Kim Jong-un, Vladimir Putin
Miongozo ya Elimu kuwafaidisha Watoto mahitaji maalum