Kiungo kutoka Ufaransa na Klabu ya Juventus ya Italia, Paul Pogba amesimamishwa kwa kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu michezoni.

Vipimo hivyo vilichukuliwa baada ya ushindi wa Juventus dhidi ya Udinese Agosti 20 na kubaini nyota huyo alitumia dawa za kuongeza nguvu.

Taasisi ya Kupambana na Matumizi ya Madawa ya Kuongeza Nguvu ya Nado ya Italia, ilisema kiungo huyo wa zamani wa Manchester United amesimamishwa kwa muda usiojulikana na sasa anasubiri hukumu yake baada ya kubaĆ­nika kutumia dawa hizo.

Juventus ilitoa taarifa ya kupokea habari za nyota wake kukutwa na hatia na kusema wanafikiria kuchukua hatua zaidi.

Hizo ni habari mbaya nyingine kwa nyota huyo anayesumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Manchester United zaidi ya mwaka mmoja uliopita.

Aliondolewa dakika za mwisho kwenye kikosi cha Ufaransa kilichokuwa kinajiandaa na fainali za Kombe la Dunia mwaka jana kutokana na majeraha ya mguu na msimu uliopita alicheza mechi sita pekee kwenye klabu yake ya Juventus.

Pogba bado hajaanza kwenye mchezo wowote msimu huu lakini ameingia mara mbili akitokea benchi na mara ya mwisho alicheza kwenye ushindi wa timu hiyo wa mabao 20 dhidi ya Empoli.

Lakini pia uchunguzi wa Polisi unaendelea Ufaransa kwamba Pogba alikuwa mwathirika wa kosa la jinai lililoanzishwa na ndugu yake Mathias ambaye alikana kuhusika.

KITAIFA: Mitumba ya Majokofu, Viyoyozi yapigwa marufuku
Kocha Simba SC apata dawa ya Zambia