Kiungo wa Inter Milan, Davide Frattesi amemuonea huruma Mlinda Lango wa Timu ya Taifa ya ltalia, Gigio Donnarumma wakati wa mechi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Ulaya (EUR0 2024) dhidi ya Ukraine baada ya mashabiki wa kumzomea.

Kiungo huyo alichukizwa na vitendo hivyo bada ya ushindi wa mabao 2-1 walioupata lakini hakufurahishwa na mashabiki walivyomzomea Mlinda Lango huyo anayekipiga Paris Saint Germain.

Mlinda Lango huyo wa zamani wa AC Milan bado anachukiwa na mashabiki kadhaa wa ltalia baada ya kujiunga na PSG lakini kiungo huyo wa Inter akasema ni aibu kubwa.

“Sijawahi kuona kitu kama hicho mchezaji wa kimataifa kuzomewa. Sijaelewa kwa nini imekuwa hivyo, wote tunawakilisha timu ya taifa, nilimfuata kipa wetu na kumwambia tunampenda hakustahili kuzomewa.

“Donnarumma ni mchezaji mkubwa sana anaweza kukabiliana na hali hiyo sidhani kama itamuathiri,” alisema Frattesi

Davide Frattesi

Donnarumma sio mchezaji maarufu tena San Siro baada ya kuondoka mwaka 2021, kipa huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa na usiku mbaya licha ya Italia kuibuka na ushindi.

Kipa huyo atarejea San Siro kuelekea mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Milan utakaochezwa Novemba 7 huku kukiwa na mashaka mashabiki wa timu hiyo huenda wakamzomea.

Ally Kamwe: Hatuna tatizo na Al Merreikh
AFCON 2023: Wapinzani wa Stars kujulikana Oktoba 12