Beki wa Arsenal, William Saliba amesema sheria mpya za Mikel Arteta zimesababisha wachezaji wa timu hiyo kuwa uhusiano mzuri zaidi nje na ndani ya uwanja.

Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa anaamini kutokana na sheria hiyo, wachezaji wa Arsenal wamejenga mawasiliano mazuri yaliyojenga urafiki, kwenye kikosi kinachowania mbio za ubingwa msimu huu.

Arteta aliandaa mpango wa kuja na sheria mpya wakati wa ziara ya kujiandaa na msimu mpya ipokwenda Marekani na imezaa matunda kwa walmujibu wa Saliba.

Arsenal ilionyesha mabadiliko kwenye ziara hiyo katika Majiji ya New York na Los Angeles baada ya sheria hiyo mpya kuanzishwa.

Saliba alielezea jinsi Arteta alivyoweza kutengeneza umoja na ushirikiano wa kukaa kiti kimoja na mtu ambaye hujamzoea wakati wa mapumziko ya kupata chakula.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 alisema kupitia chombo cha habari cha klabu hiyo: “Kocha mara nyingi anazungumza na sisi kuhusu umoja na kuwa pamoja, sio tu mashabiki hata kwenye timu, mfano tulipokuwa kwenye ziara Marekani.

Wakati wa kula kocha anabadilisha meza. Hatuchagui mtu wa kukaa naye wakati wa kula chakuka cha mchana au usiku. Amefanya hivyo ili kuwa na uhuru wa kuzungumza na kila mtu na nimeipenda sana bila sheria. Hiyo inasaidia kuongea na mtu ambaye hazungumzi naye kila mara,” alisema Saliba

Robertinho awakomalia Chama, Phiri
Ally Kamwe: Hatuna tatizo na Al Merreikh