Mabingwa wa Soka nchini Hispania ‘La Liga’ FC Barcelona wanajiandaa katika vita kupigania kumsajili Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka nchini England Manchester City, Erling Haaland.

Kwa muda mrefu Real Madrid imekuwa ikichukuliwa kama timu inayomfaa zaidi Haaland, lakini sasa kwa mujibu wa tovuti ya michezo 90min, Barca inajiandaa kufanya harakati kumsajili mshambuliaji huyo mahiri, raia wa Norway.

Kwa sasa Barca ina Robert Lewandowski anayeongoza safu ya ushambuliaji, lakini katika mpango wa muda mrefu, Haaland anaonekana chaguo linalofaa kuwa mbadala wa mkongwe huyo wa Poland, ambaye hivi karibuni alitimiza miaka 35.

Mapema mwezi huu ripoti zilisema City inapanga kumpatia Haaland ofa ya mshahara wa pauni 600,000 kwa juma ikihofia huenda akarubuniwa ahamie klabu za Saudi Arabia au Read Madrid.

Haaland ameng’ara City tangu alipowasili msimu uliopita akitokea Borussia Dortmund kwa mkataba wa miaka mitano akisaidia timu hiyo kutwaa mataji matatu ambayo ni Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu England na Kombe la FA.

Pia Haaland alishinda kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu England na cha Ulaya na pia alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Ulaya akimpiku, Lionel Messi.

Kwa jumla Haaland mwenye umri wa miaka 23 amefunga mabao 52 katika mashindano yote msimu uliopita yakiwamo 36 aliyoweka rekodi kwenye Ligi Kuu England.

Hassan Mwakinyo kupambana na Kiduku
Mnyama anamfuata Power Dynamos