Kiungo Mshambuliaji ‘WINGA’ Manchester United, Jadon Sancho anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo wakati wa dirisha dogo la uhamisho ifikapo Januari, 2024 baada ya kushindwa kumaliza tofauti zake na Kocha, Erik ten Hag.

Sancho amefanya mazungumzo na Ten Hag kuhusu hatima yake United kufuatia kurushiana vijembe kati yao majuma mawili yaliyopita baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Arsenal.

Ten Hag alimwondoa winga huyo wa England kwenye kikosi kilichopokea kipigo dhidi ya Arsenal na akieleza mtazamo mbaya na uvivu kwenye mazoezi wa Sancho kuwa ndio sababu za maamuzi hayo.

Sancho alijibu kupitia mitandao ya kijamii akikanusha madai hayo na kumshutumu Ten Hag kwa kusema uongo.

Ripoti zimesema hata kukosekana kwa sasa kwa winga mwenzake, Antony kutokana madai ya unyanyasaji wa wanawake ambayo amekanusha, hakutarajiwi kuongeza nafasi ya Sancho kurejea kwenye kikosi cha kwanza.

Manchester United ilimsajili Sancho mwenye umri wa miaka 22 mwaka 2021 kutoka Borussia Dortmund kwa ada ya uhamisho ya dola milioni 87.94.

Declan Rice afunguka anaowahusudu
Hassan Mwakinyo kupambana na Kiduku