Kiungo mpya wa Arsenal, Declan Rice, amemtaja kiungo wa Manchester City, Rodri kuwa ni mchezaji ambaye amekuwa akimuangalia zaidi.
Rice ni moja kati ya viungo bora katika Ligi ya England ‘Premier League’ ambapo msimu huu amejiunga na Arsenal akitokea West Ham United kwa uhamisho wa dau la Pauni 100m.
Rodri msimu uliopita alitisha akiwa na Man City wakati wakitwaa mataji matatu, Premier League, Ligi ya Mabingwa na Kombe k FA. Pia alikuwa mcheza bora wa UEFA, huku akiiongoza Hispania kutwaa UEFA Nations League.
Rice alinukuliwa akisema: “Kwa Premier League, Rodri kwangu ndiye bora kwa wachezaji wa nafasi yangu.
“Ni mchezaji ambaye anajituma, napenda aina ya uchezaji wake, niseme tu yeye ni mchezaji wa daraja la juu.”
Rice aliendelea kufunguka kuhusiana na kiungo mwenzake wa Arsenal, Thomas Partey na yule wa Real Madrid, Aurelien Tchouaméni akisema: “Nilipokuja Arsenal, Partey alikuwa moto mpaka anaumia, yuko vizuri. Kwa upande wa Tchouaméni bado kijana ila akiwa na mpira amekuwa akifanya vizuri.
“Kwa sasa najaribu kujifunza kutoka kwa kila mtu, nina miaka 24, ni wakati wa kupambana na kuna vitu natakiwa kujifunza.”