Beki wa Manchester United, Harry Maguire ameweka kuwa anajipanga kwa ajili ya kupambania nafasi yake ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo chini ya kocha Eric ten Hag.

Maguire ameongeza kuwa hana shida ya kutocheza baadhi ya michezo kwa kuwa anaamini bado kuna mechi nyingi ambazo atapata nafasi ya kucheza.

Maguire alisema: Majuma manne ya kwanza yalikuwa magumu, kwa sababu kulikuwa na mechi moja na kocha hakunichagua kucheza lakini kuna mechi nyingi zinakuja, nina imani nitacheza.

Najua kutakuja stori kwangu, lakini nataka kucheza, ninataka tena kucheza mpira na nitapambana kwa ajili ya hilo.

West Ham?

Hawakuja kwa ajili ya makubaliano. Man United wana furaha kwa ajili yangu na mimi nina furaha kuwa hapa, nitapambana kwa ajili ya nafasi yangu kwa kuwa niko tayari.”

Waliosababisha vifo watu sita wasakwa na Polisi
Aubun Kramo akomalia kurudi kwao