Hofu iliyotokana na tukio la Paul Pogba kugundulika kutumia dawa ya kusisimua misuli imesababisha Mkurugenzi wa michezo wa Juventus, Cristiano Giuntoli kutafuta viungo wa kuziba pengo lake.

Kwa mujibu wa mtandao wa michezo Calciomercato wa Italia, miamba hiyo ya Serie A imeorodhesha wachezaji kadhaa inaoona wanafaa kuchukua nafasi hiyo.

Kiungo wa Washika Bunduki wa Kaskazini mwa jijini London ‘Arsenal’ Thomas Partey anapewa nafasi ya kwanza katika orodha hiyo, huku wakiripotiwa kuwa tayari kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kuondoka pale Emirates.

Khephren Thuram wa Nice ni mchezaji mwingine ambaye Giuntoli anaona kivutio, lakini pia anaweza kuwa ghali zaidi kwenye orodha hiyo kwa kuwa na thamani ya euro milioni 35.

Juve pia inasaka saini ya Manu Kone wa Borussia Monchengladbach, ambaye awali aliwasiliana AC Milan wakati akikiwasha Toulouse ya Ufaransa na amekuwa katika kiwango bora tangu alipohamia Bundesliga.

Kiungo wa Strasbourg, Habib Diarra ndiye anayefuata katika orodha hiyo, lakini Juve inaweza kukabiliwa na ushindani mkubwa kutoka Wolfsburg katika kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 19 anayekadiriwa kuwa na thamani ya Euro milioni 20.

Mchezaji wa mwisho katika orodha hiyo ni Abdoulaye Kamara kutoka Borussia Dortmund, ingawa Juve inataka kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 18 kama tegemeo la baadaye kuliko wa kikosi cha kwanza kwa sasa.

Gharama za maisha pasua kichwa, Waziri ajitetea
Washauri Vijana wapewe nafasi kuijenga Demokrasia