Serikali nchini India, imewaweka chini ya uangalizi maalum Wahudumu wa afya 153, kufuatia vifo vya watu wawili waliokuwa wakiwahudumia na ambao  waliopoteza maisha kwa kirusi cha Nipah.

Mbali na watu hao wawili kupoteza maisha, pia zaidi ya watu 700 wanafanyiwa vipimo kubaini iwapo wameambukizwa ugonjwa huo usio na chanjo, na tayari India, imezuia mikusanyiko ya watu na kufunga baadhi ya shule katika jimbo la kusini la Kerala.

Virusi hivyo, vinadaiwa kuambukizwa kutoka kwa Popo au Nguruwe, ambapo mtu hupata homa kali, kutapika, kushindwa kupumua na hata kupelekea ugonjwa wa kupooza.

Tayari Watu watatu wamegundulika kuambukizwa virusi hivyo huku wengine zaidi ya 700 wakiwemo wafanyakazi hao wa afya 153 wakitengwa kwa ajili ya uangalizi  zaidi.

Kamchape waingia kwenye 18 za Polisi Katavi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 17, 2023