Askari wa Kike wa Tanzania, wameshiriki Mkutano wa mwaka 2023 wa Mtandao wa Polisi Wanawake Duniani – IAWP, Nchini New Zealand, ukiwa umebeba kaulimbiu isemayo “Refresh, Renew, Refocus” na ambao umefunguliwa hii leo September 17, 2023 jijini Auckland.

Aidha, mbali na Tanzania Mkutano huo pia umeudhuriwa na mataifa mengine ikiwemo la Ghana na Afrika Kusini, ambapo mafunzo ya mkutano huo pia yanalenga kuwajengea uwezo Askari wa kike, sambamba na kutoa fursa na kutengeneza mtandao wa mawasiliano kwa wasimamizi wa sheria.

Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa mwezi Julai, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano kama huo kwa ukanda ya Afrika uliyofanyika jijini Dar es Salaam na kuleta matokeo makubwa ya kiutendaji kwa Maafisa na Askari wa kike ambao walishiriki mada mbalimbali kwa lengo la kuwaongezea uwezo na maarifa ya kiutendaji.

Ujumbe wa Askari wa kike kutoka Tanzania umeongozwa na Kamishna wa Polisi, CP Suzan Kaganda wa kamisheni ya Utawala na rasilimali watu na  umetumia mkutano huo kutangaza utalii na vivutio vya kitamaduni vilivyopo Tanzania na utahitimishwa Septemba 21, 2023.

Waliofariki kwa mafuriko Libya wafikia 11,300
Madaktari wa dharula 35 wapelekwa Libya