Maelfu ya watu Nchini Marekani, wamekusanyika jijini New York wakishinikiza kuongezwa kwa juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo kusitisha matumizi ya Petroli.

Mkusanyiko huo, uliratibiwa na Taasisi 700 na makundi ya Wanaharakati, ikiwa ni siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unaotarajiwa kuhudhuriwa na Rais qa Taifa hilo Joe Biden.

Baadhi ya Watu waliojitokeza katika maandamano ya Wanaharakati wa mazingira jijini New York. Picha ya Bryan Woolston/AP.

Waandamanaji hao, walifurika kwenye mitaa kadhaa ikiwemo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa – UN, wakati Viongozi wa Mataifa Duniani wakiwasili kuhutubia hadhara kuu ya umoja huo, hapo kesho siku ya Jumanne Septemba 19, 2023.

Aidha, jumbe zilizoandikwa kwenye mabango hayo ziliakisi mchango hasi wa Nishati ya Petroli katika uchafuzi wa mazingira na pia kukumbusha jinsi mabadiliko ya tabianchi yanavyoongeza majanga ya asili, kama moto na mafuriko.

Jiepusheni na mikopo kausha Damu - Kikwete
Polisi yawashukia wanaojichukulia sheria mikononi