Ofisi ya Makamu wa Rais, imesema itaendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari nchini katika kutoa elimu kwa umma, kuhusu umuhimu wa uhifadhi na utunzaji wa mazingira, ikiwemo wa uhifadhi wa Tabaka la Ozoni.

Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Mitawi, wakati akifungua warsha ya mafunzo kwa Waandishi wa Vyombo vya Habari kuhusu udhibiti wa uingizaji wa Kemikali zinazodhibitiwa chini ya Itifaki ya Montreal, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Amesema, Tanzania imeendelea kuwa mstari wa mbele katika kukabiliana na athari za matumizi vifaa vya Kemikali vyenye ukomo wa matumizi kwa kuimarisha mifumo ya udhibiti wa kemikali hizo, ambazo zina madhara mbalimbali katika jamii, ikiwemo magonjwa, ongezeko la joto duniani na mabadiliko ya tabianchi.

“Tutaendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari katika kuhakikisha elimu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira inaifikia jamii. Tunatambua mchango mkubwa wa JET kwani tangu kuanzishwa kwake mwaka 1991 imekuwa mstari wa mbele kuhamasisha jamii kutunza na kuhifadhi mazingira,” amesema Mitawi.

Chama: Tumalizane na Coastal Union kwanza
Jiepusheni na mikopo kausha Damu - Kikwete