Kocha Mkuu wa Liverpool Jurgen Klopp amefichua kwamba Alexis Mac Allister alijisikia nafuu kwa kutolewa nje baada ya kikosi chake kufanya vibaya kipindi cha kwanza katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Wolves juzi Jumamosi (Septemba 16).

Wekundu hao wa Anfield walikuwa bila Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold, wakati Hwang Hee-chan alipofunga baada ya kazi kubwa kutoka kwa Pedro Neto na walikuwa na wakati mgumu wa kutengeneza nafasi katika kipindi cha kwanza.

Mac Allister alikuwa na dakika 45 za kwanza baada ya kusafiri hadi Amerika Kusini kuichezea Argentina wakati wa mapumziko ya kimataifa, alipewa kadi ya njano mapema.

Kiungo huyo wa zamani wa Brighton, nafasi yake ilichukuliwa na Luis Diaz na Liverpool walisawazisha dakika ya 55 kupitia kwa Cody Gakpo kabla ya Andy Robertson kumalizia kwa akili na bao la kujifunga la Hugo Bueno kumpa Klopp ushindi wa mabao 3-1.

Klopp alikiri baada ya mabadiliko ya mchezo kuhitajika wakati wa mapumziko ili kuwarudisha Liverpool mchezoni, badala ya Mac Allister kuwa mmoja wao baada ya ratiba ngumu ili- yojaa safari.

Alisema: Jambo zuri katika kipindi cha kwanza ni kwamba ilikuwa mbaya kiasi kwamba sikufikiria kwamba tunaweza kucheza kipindi cha pili namna hiyo.

“Ni wazi tulitaka kuanza tofauti kabisa, lakini kwa sababu yoyote haikuwezekana.

“Kiwango kilikuwa chini. Hatukuweza kubadilika mara tano wakati wa mapumziko, kwa hiyo tulidhani tungebadilisha mfumo.

“Alikuwa na wakati mzuri katika kipindi cha kwanza, lakini hakukatishwa tamaa kuondoka, alipata nafuu zaidi.”

Wachezaji wengine wa akiba Darwin Nunez na Harvey Eliott walisaidia Liverpool kushikilia zaidi mechi hiyo baada ya kipindi cha kwanza.

Gamondi asitisha shangwe Young Africans
Chama: Tumalizane na Coastal Union kwanza