Mshambuliaji kutoka nchini Ureno Joao Félix, amesema anafurahia maisha ndani ya Barcelona baada ya kufunga bao lake la kwanza katika ushindi wa mabao 5-0 Jumamosi (Septemba 16) dhidi ya Real Betis kwenye Ligi Kuu Hispania, La Liga.

Félix, ambaye alijiunga na Barca kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Atletico Madrid mwezi huu, alifunga bao la kwanza kwenye Uwanja wa Olympic na kisha alitumia vizuri pasi ya Andreas Christensen na kusaidia kutengeneza bao la Robert Lewandowski.

Ferran Torres, Raphinha na João Cancelo pia walifunga wakati Barca ikipaa kileleni mwa La Liga kwa muda kabla ya mchezo wa Real Madrid dhidi ya Real Sociedad uliopigwa jana Jumapili (Septemba 17).

“Nina furaha sana kuanza kikosi cha kwanza, hisia ni nzuri sana ni rahisi kucheza katika timu hii,” alisema Felix, ambaye alitumia kipindi cha pili cha msimu uliopita kwa mkopo kule Chelsea.

“Unapokuwa na muundo mzuri na kuzunguka mpira kwa kasi, nafasi zinaonekana na pia mabao. Nina furaha, mabadiliko yamenifanya vizuri, mimi na familia yangu, nina furaha sana hapa.”

Félix mwenye umri wa miaka 23, ameungwa mkono na kustawi Barca baada ya misimu minne ya kupanda na kushuka kule Atletico kutokana na uhamisho wake wa Euro milioni 126 kutoka Benfica ya Ureno mwaka 2019.

Vyombo vya habari vya ndani vimependekeza mtindo wa Barca utamfaa zaidi, ingawa kocha Xavi Hernandez hakutaka kuhusishwa na kulinganisha na Atletico, akisema “namheshimu sana” kocha wao, Diego Simeone.

Hata hivyo, Xavi aliwamwagia sifa wachezaji wawili waliosajilwa hivi karibuni na Barca, huku Cancelo, ambaye amejiunga kwa mkopo kutoka Manchester City.

“Joaos wote wana furaha hapa na unaweza kuona hilo,” Xavi alisema katika mkutano na wanahabari.

“Hakuna anayetilia shaka ubora wao binafsi. Unawaona wakifanya mazoezi na unaona jinsi walivyo wazuri.

“Cancelo anajiunga nasi baada ya kufanya kazi na kocha bora zaidi duniani (Pep Guardiola) na anautafsiri mchezo vizuri sana. Anaelewa tunachotaka.

“Wote Cancelo na Félix wanatoachaguzi zinazosaidia kuboresha timu. Kimwili, wako imara. Wanaongeza ubora kwenye kikosi. Wako pale wanapotaka kuwa.”

Kumbe Hersi Said alifanya kufuru Kigali-Rwanda
Robertinho awasubiri kwa hamu Power Dynamos