Baadhi ya watu Ulimwenguni yakiwemo mashirika ya kutetea haki za Binadamu, yamekuwa yakipinga uwepo wa adhabu ya Kifo wakidai ni jambo ambalo linaondoa haki ya binadamu kuishi na lililo kinyume na fikra za wabobezi wa masuala ya kidini.

Hayo yamebainishwa na Sheikh Mussa Kundecha, wakati akifanya mahojiano maalumu na Dar24 Media na kuongeza kuwa pia Dunia imekuwa ikikabiliwa na hofu juu ya Mwanamke na kudhani hatendewi haki kitu ambacho jamii inapaswa kukitafutia ukweli.

Amesema, “hiyo ni hofu, na namna hofu inavyowatesa wengi na kusema kuwa mtu anatakiwa kuogopa kosa alilotenda ni kwasababu tu anaona atapata adhabu fulani, hofu yako juu ya adhabu hiyo itatokana na kosa lako, kwahiyo usihofu adhabu ile maana kuna adhabu ya kifo.”

Sheikh Kundecha ameongeza kuwa, “hata Quruani imezungumzia hofu katika maeneo mengi ambapo eneo moja Mungu amesema msiwaogope watu kwa chochote kile niogopeni mimi, hadithi ya Mtume Mohamed inasema asihofu mtu kitu chochote duniani hofu aliyonayo aiweke kwenye makosa anayofanya.”

Aidha, ameongeza kuwa watu wanakufa kwa matukio ya mbalimbali, ikiwemo ajali, akisema “huwezi acha kusafiri eti kwasababu kulitokea ajali, wanazama kwenye meli, ajali za ndege au kimbunga, hatuwezi kuogopa kukaa kwasaabu kuna upepo kuna dhoruba kuna magonjwa, hizi zote ni hofu kwa hivyo usiohofie mambo haya hofia usalama,” amesema Kundecha.

Mwalimu mbaroni kwa kumbaka Mwanafunzi
Ukusanyaji Kodi: Maofisa KRA kupita nyumba kwa nyumba