Ripoti ya Umoja wa Mataifa – UN, imeeleza kuwa zidi ya Watoto 1,200 wanadaiwa kufariki katika kambi za wakimbizi nchini Sudan tangu mwezi Mei 2023, huku Watoto wachanga wakikabiliwa na tishio la vifo.

Kwa mujibu wa Msemaji wa UN linaloshugulikia maslahi ya watoto la UNICEF, James Elder amesema inahofiwa kuwa watoto nchini Sudan watafariki kati ya sasa hadi mwishoni mwa mwaka, kutokana na sababu mbalimbali za kiafya na machafuko.

Kambi hizo zilikuwa zinatoa hifadhi kwa wakimbizi kutoka katika mataifa ya Sudan Kusini na Ethiopia
Kambi ya Wakimbizi nchini Sudan. Picha ya Jok Solomun / Reuters.

Amesema Watoto 333,000 wanatarajiwa kuzaliwa nchini Sudan kati ya mwezi Oktoba na Desemba 2023, huku pia akielezea wasiwasi wake kuhusu hali ya kiafya nchini haswa kwa watoto kutokana vita vinavyoendelea.

Hali hiyo, inatukiwa huku UNHCR ikieleza kuwa Wafanyakazi wake katika jimbo la White Nile walikuwa wamesajili vifo vya zaidi ya Watoto 1,200 kati ya Mei 15 na Septemba 14, 2023 katika kambi tisa za Wakimbizi Nchini Sudan.

Wizara yalaani tukio kuteswa kwa Mtoto, wahusika wasakwa
Kashfa: Polisi 1,000 wasimamishwa kazi