Wakati Azam FC ikishuka dimbani kesho Alhamis (Septemba 21) dhidi ya Singida Fountain Gate, Kocha wa timu hiyo, Yusuph Dabo amesema kikosi chake kinapaswa kujituma zaidi, kuendelea kung’ara msimu huu 2023/24.

Azam FC itachuana na Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.

Timu hiyo itaingia katika mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mechi zake mbili zilizopita za michuano hiyo msimu huu.

Azam FC ilianza ligi hiyo kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tabora United kabla ya kushinda mabao 3-1 ilipocheza na Tanzania Prisons.

Akizungumzia mchezo ujao dhidi ya Singida Fountain Gate, Dabo ambaye ni raia wa Senegal, amesema lengo lake ni kuona timu yake ikipata ushindi katika kila mchezo.

Kocha huyo amesema wachezaji wake wanapaswa kujituma katika kila mchezo kuhakikisha lengo la ushindi linakamilika.

Harry Kane aipandisha Presha Man Utd 

“Ni muhimu kwa wachezaji kucheza kwa kujitoa zaidi kupata matokeo mazuri, tutaendelea kuyafanyia kazi makosa mbalimbali yanayojitokeza ili tuwe imara zaidi,” amesema.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Azam FC inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi sita baada ya kushuka dimbani mara mbili.

Guardiola atamba kutetea ubingwa wa Ulaya
Harry Kane aipandisha Presha Man Utd