Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inapanga mkakati wa kuanza kuifanyia kazi changamoto iliyopo Mkoani Lindi ya uwepo Ndovu, ambao huharibu mazao na kujeruhi wananchi, huku akiwataka amewataka Viongozi kubuni mkakati wa kitaifa ili kutatua migogoro ya Wakulima na Wafugaji.

Rais Samia amesema hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Lindi iliyopo kijiji cha Mitwero, na kudai kuwa mkakati huo unalenga kudhibiti ndovu, ili kulinda usalama wa maisha na mali za wananchi.

Muonekano wa Ujenzi wa Bandari ya Uvuvi iliyopo Kilwa Masoko Mkoani Lindi ambapo jiwe la msingi la ujenzi huo limewekwa na Rais Dkt. Samia Suhuhu Hassan Septemba 19, 2023.

Kati aziara hiyo, Rais Samia pia aliweka Jiwe la Msingi mradi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa Masoko inayotarajiwa kukamilika Februari 2025 kwa gharama ya shilingi bilioni 266 na unaotarajia kutoa ajira zaidi ya 30,000, huku akizindua awamu ya kwanza ya ugawaji wa Boti za kisasa.

Katika awamu hiyo, jumla ya Boti 160 za mkopo nafuu zitagawiwa kote nchini kwa ajili ya uvuvi na kilimo cha mwani ambapo pia Rais Samia aliweka Jiwe la Msingi kwenye shule ya sekondari wasichana Lindi, iliyoko kijiji cha Kilangala ikiwa ni moja kati ya shule 10 zinazojengwa chini ya Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP).

Aubin Kramo kupasuliwa Goti
Guardiola atamba kutetea ubingwa wa Ulaya