Mlinda Lango wa zamani wa Manchester United, David De Gea huenda akajiunga na Real Betis baada ya kuwa nje ya uwanja tangu alipoachana na Mashetani Wekundu msimu uliopita.

Nyota huyo amekataa ofa nyingi tangu mkataba wake ulipomalizika Old Trafford, Juni mwaka huu baada ya kuhusishwa na klabu kubwa kama Bayern Munich na Real Madrid.

Hata hivyo, De Gea anaweza kurejea Hispania akaendeleze soka lake baada ya kuondoka England alikoishi kwa miaka 12.

Inaelezwa kwamba Valencia ilionyesha nia ya kumsajili kipa huyo mwenye umri wa miaka 32, lakini Betis imeonckana kuwa mstari wa mbele baada ya mazungumzo na kipa wa zamani wa Manchester City, Claudio Bravo kuvunjika.

Inasemakana De Gea anathamini ofa iliyotolewa na Betis baada ya kuzipiga chini timu nyingine ambazo zilionyesha nia ya kumsajili.

Awali, Inter Milan pia ilimfikiria De Gea kama mbadala wa Andre Onana baada ya kipa huyo kujiunga na Man United kwenye dirisha la usajili la kiangazi.

Hata hivyo ilimpotezea, huku De Al-Nassr ya Saudi Araumu bia nayo ilimnyemelea.

Licha ya De Gea kutopata timu kwenye dirisha la usajili lililopita ameendelea kujifua ili kujiweka fiti baada ya kukaa nje tangu Juni.

Mashabiki wamekuwa wakimpa sapoti De Gea aongeze juhudi kupitia mitandao ya kijamii baada ya kuweka picha mbalimbali za mazoezi.

Ramani ya kutinga Makundi kuchorwa Chamazi
Young Africans yawaingiza chaka Al Merreikh