Afarah Suleiman – Manyara.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, limesema kwa kipindi cha miezi sita wamekamata makosa ya usalama barabarani 20,905 na kesi 47 zimefikishwa Mahakamani ambazo zilikutwa na hatia na kuwafungia madereva wawili wa mabasi kwa kosa la uendeshaji wa hatari.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna msaidizi wa Polisi, George Katabazi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, ambapo pia limewataka Madereva na watumiaji wengine wa Barabara kufuata taratibu na Sheria za usalama barabarani, ili kuzuia ajali za mara kwa mara.

Amesema, pia wamehakiki wa leseni 772 na leseni 91 kati ya hizo zilibainika kutokuwa na sifa na kwamba Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linaendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia dhana ya ulinzi shirikishi, ili kupunguza uhalifu ikiwemo makosa ya barabarani.

Wakati huo huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Stella Mutabihirwa amewataka Wakuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya zote Mkoa wa Singida kuhakikisha wanaambatana na timu ya watalamu wa ukaguzi wa matukio kisayansi (FBI), pindi wanapokwenda kukagua maeneo ya uhalifu, ili kurahisisha na kuharakisha upelelezi wa kesi.

Young Africans yawaingiza chaka Al Merreikh
Julian Nagelsmann anukia Ujerumani