Miamba ya Soka nchini Ujerumani, FC Bayern Munich leo Jumatano (Septemba 20) wanatarajia kumkosa kocha wao Mkuu, Thomas Tuchel wakati ambao watakuwa wanapambana na Manchester United kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ‘UEFA’.

Bayerm watamkosa kocha wao huyo kutokana na kutumikia adhabu ya kadi nyekundu ambayo aliipata msimu uliopita kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Manchester City ikiwa ni baada ya kulumbana na mwamuzi wa pembeni kwenye mchezo huo.

Kutokuwepo kwa kocha huyo kunaweza kuwa pigo kwa klabu hiyo kwa kuwa walikuwa wanamuhitaji katika kukiongoza kikosi hicho katika kusaka pointi tatu mbele ya wapinzani wao, ikizingatiwa hawakupata matokeo mazuri kwenye nchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu Ujerumani ‘Bundesliga’ baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Bayer Lervekusen.

Hata hivyo Bayem wanajivunia juu ya uwepo wa Mshambuliaji wao, Harry Kane ambaye anaijua vilivyo timu hiyo kwa kuwa alikuwa akicheza ndani ya Premier ambapo inatokea Man United ambayo kwenye mchezo huu wana kazi ya ziada ya kufanya kwa kuwa mechi zao mbili zà mwisho walipoteza zote dhidi ya Arsenal na Brighton.

Phiri, Baleke wanyooshewa kidole Simba SC
Kocha Azam FC afunguka pengo la Sebo