Katika kuendelea kudumisha dhamira ya ubunifu wa kiteknolojia, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited – GGML, imetoa Shilingi milioni 150 kudhamini Maonesho ya sita ya Teknolojia ya Madini yanayofayika mkoani Geita na yanayotarajiwa kuzinduliwa Sepemba 23 na kuhitimishwa Septemba 24.

Maonyesho hayo ya kila mwaka, yanafanyika kwa ushirikiano kati ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania – TANTRADE, katika viwanja vya Bombambili vilivyopo eneo la Mamlaka ya Maeneo ya Usindikaji Nje – EPZA, Mkoani humo.

Meneja Mwandamizi anayesimamia Mahusiano Jamii, Gilbert Mworia alisema maonesho hayo yamekuwa na mvuto wa kipekee tangu yalipoasisiwa kutokana na ufadhili wa GGML kupitia mfuko wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) ambao uliwezesha ujenzi wa eneo hilo la EPZA pamoja na eneo la uwanja huo wa maonesho.

Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong (kulia) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kitengo cha huduma za dharura cha kampuni hiyo pindi waliposhiriki maonesho hayo mwaka jana. Kushoto ni Makamu Rais wa AngloGold Ashanti- GGML anayesimamia miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo.

Amesema, “mbali na maonyesho, tuliwekeza Sh 800 milioni katika ujenzi wa jengo la utawala la EPZA. Tunafurahi kuona mpango wetu wa EPZA mkoani Geita unastawi na kutimiza malengo ya jamii ya wana-Geita kikamilifum saada wetu tumeendelea kuutoa kila mwaka ikiwemo maandalizi ya maonesho hayo,” alisema Mworia.

Aidha ameongeza kuwa, katika kipindi cha miaka sita ya ushirikiano huo na wadau wa maonesho hayo, GGML imeendelea kuelimisha jamii kuhusu teknolojia inayotumika katika vifaa vya uchimbaji madini hali inayoendelea kukuza uhusiano imara kati yake, kampuni za ndani na wachimbaji madini.

Aidha, alisema ili kutimiza malengo ya muda mrefu ya ukuaji wa uchumi endelevu, GGML inaunga mkono Dira ya 2025 ya serikali. Mpango huu unalenga kuiwezesha sekta ya uchimbaji madini kukua na kufikia kiwango cha asilimia 10 kwenye Pato la Taifa la Tanzania.

Ufunguzi rasmi wa Maonesho hayo ya 6 ya Madini na Teknolojia Mkoani Geita yenye kauli mbiu “Matumizi ya teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira” utafanywa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Dotto Biteko Septemba 23 na kufungwa na Septemba 30, 2023 na Rais Samia Suluhu Hassan.

Simba, Young Africans zapewa NONDO kimataifa
Siri za Mo Salah zaanikwa hadharani