Mahakama ya Mkoa wa Vuga, imemhukumu mshtakiwa Khamis Ali Othamn (25), kifungo cha miaka 25 Chuo cha Mafunzo (Jela), sambamba na kulipa fidia ya Shilingi 500,000 kwa kosa la shambulio la aibu.

Akisoma maelezo ya hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama, Taki Abdallah amesema amejiridhisha na ushahidi uliotolewa ambao haukuwa na chembe ya shaka uliomtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa hilo.

Awali, Khamis alishtakiwa kwa kosa la shambulio la aibu kwa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka nane ambapo Mshtakiwa alimchezea sehemu za siri za mbele za mtoto huyo, jambo ambalo ni kosa kinyume na kifungu namba 114(1) cha sheria ya adhabu namba 6/2018 Sheria ya Zanzibar.

Kesi hiyo, ilikuwa na Jumla ya mashahidi wanne walitoa ushahidi mbele ya Mahakamani dhidi ya mtuhumiwa huyo Mshirazi na mkazi wa Mwera Zanzibar, ambaye amehukumiwa hii leo Septemba 20, 2023 na kesi hiyo ilifunguliwa Mahakamani Julai 17, 2023 na kupewa namba 109/2023.

Mwendokasi Mbagala - Vikindu mbioni kujengwa
Simba, Young Africans zapewa NONDO kimataifa