Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ wanaripotiwa kuonyesha nia ya kutaka kumsajili Mshambuliaji wa Real Madrid, Rodrygo ili kuziba pengo ambalo huenda likaachwa Mohamed Salah, ambaye inaandamwa na taarifa za kutimkia Al- Ittihad ya Saudi Arabia.

Al-Ittihad waliitetemesha Liverpool majira ya joto mwaka huu baada ya kuonyesha nia ya dhati kumhitaji Salah inaonekana wazi wanaweza kurejea tena kwenye usajili mdogo wa Januari na sasa Majogoo hao wameshtuka wanaanza kujiandaa.

Rodrygo, ambaye ana umnri wa miaka 22, ameanza kwenye mechi zote tano za Real Madrid za La Liga msimu huu na vyombo vya habari Hispania vinadai klabu hiyo itakuwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya staa huyo hasa kutokana na uwezekano mkubwa wa Kylian Mbappe kutua majira ya joto mwakani.

Inadaiwa Madrid itatamuachia winga huyo kwa dau linalotajwa kuwa euro mil 100 wakiamini ndio thamani yake kwa sasa.

Ahmed Ally amjibu Julio na wenzake
Inonga yupo sawa, aombwa radhi