Shujaa wa Inter Miami, Lionel Messi huenda akakosa fainali ya U.S Open Cup dhidi ya Houston Dynamo, pia hatakuwapo kwenye mechi yao ijayo ya ligi dhidi ya Orlando City itakayochezwa keshokutwa Jumapili (Septemba 24), kwa mujibu wa kocha Tata Martino.

Messi alirejea dimbani baada ya mechi za kimataifa za kufuzu Kombe la Dunia alikoenda kukitumikia kikosi cha Argentina, hata hivyo hakuweza kuendelea na mechi dhidi ya Toronto na kocha wake akamtoa.

Jordi Alba ambaye alikosa mechi ya mwisho ya Inter Miami alifanyiwa mabadiliko mapema dhidi ya Toronto usiku wa kuamkia jana (Jumatano) kama Messi huku Inter Miami ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mastaa hao wa zamani wa FC Barcelona watafanyiwa uchunguzi siku chache zijazo na huenda wakapumzishwa kwanza kabla ya fainali hiyo itayochezewa Septemba 27.

“Tutafuatilia kila siku ripoti za madaktari tuone watakachotuambia. Tunaendelea kuwa karibu nao lakini sidhani kama watacheza Jumapili, Messi ana jeraha la muda linalomsumbua, hana maumivu ya msuli. Ndio maana tukampumzisha dhidi ya Atalanta. Nimeongea kama kocha kwa sababu mengi yalizungumzwa.

Messi alikuwa na mehango mkubwa tangu alipojiunga Inter Miami akiisaidia kubeba ubingwa wa Kombe la Ligi kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo na alifunga mabao 11 katika mechi 12 alizocheza tangu alipojiunga nayo.

Fedha za Wadau zitatue changamoto za jamii - Dkt. Mollel
JKT Tanzania yaipeleka Kagera Sugar Shinyanga