Mchungaji wa Kanisa la Wellspring of God Ministry, Agbarha-Otor la Nchini Nigeria, Alex Itedjere anadaiwa kumuua msichana mdogo aliyepotea kwa majuma kadhaa ka jamii ya Agbarha-Otor, eneo la Serikali ya Mtaa wa Ughelli uliopo Kaskazini mwa Jimbo la Delta kwa sababu ambazo bado hazijawekwa wazi.

Mchungaji huyo, inasemekana kuwa alimuua binti huyo katika makazi yake huku mabaki ya mwathiriwa yakipatikana katika ndani ya chumba kimojawapo cha nyumba ya mtumishi huyo aliyeacha utata na maswali kwa wakazi wa eneo hilo na waumini wake kiujumla.

Mchungaji wa Kanisa la Wellspring of God Ministry, Agbarha-Otor Alex Itedjere.

Ingawa hakuna maelezo zaidi wala hali ilivyokuwa kuhusu kifo cha msichana huyo, bado nia ya kitendo kilichofanywa na Mchungaji huyo haijajulikani, ingawa inasemekana kuwa alitumia Panga kutekeleza tukio hilo lililoacha vilio, simanzi na majonzi kwa jamii.

Polisi katika eneo hilo, imelazimika kuingia kazini kutuliza ghasia baada ya Vijana wenye hasira katika jamii anayotokea Msichana huyo, kujitokeza hadharani wakifanya fujo na kulipiza kisasi, wakidai wanataka kumuuwa Mchungaji huyo ambaye tayari anashikiliwa kwa mahojiano.

Makamu Rais GGML atembelea maonesho ya madini Geita
Serikali yatenga Bil. 11 ujenzi wa Miundombinu