Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah, amewataka wananchi wa Kijiji cha Msomera cha Wilayani Handeni kuendelea kudumisha mila na desturi zao na kutokubali kuchonganishwa na Serikali.

Rajabu ametoa rai hiyo hii leo Septemba 23, 2023, wakati wa tamasha la burudani la kudumisha mila na tamaduni za jamii ya wakulima na wafugaji linalofanyika katika kijongoji cha Oromoti na kudai kuwa CCM imefanya mambo mengi mazuri ina ilani inayotekelezeka kupitia miradi ya maenedeleo.

“Na katika uchaguzi ujao wa vijiji na vitongoji vyote vya Mkoa wa Tanga, hatutapoteza hata kimoja, uchaguzi Mkuu wa 2025 majimbo 12 yote yatakuwa ya CCM na Rais Samia atapata kura nyingi kuliko mtu yeyote ndani ya nchi kwani ilani ya 2020/25 imetekelezwa vyema na CCM ina sera nzuri zinazotekelezeka.”

Katika hatua nyingine, Wakazi wa Mji wa Msomera, wamemsimika Rajabu kuwa Chifu wao na kumuomba awe anawatatulia changamoto zitakazojitokeza huku mmoja wa Wakazi wa mji huo, Kanio Olengai, akimshukuru Rais Samia kwa kuwaleta katika mazingira mazuri ya kuishi tofauti na walivyokuwa wakiishi Ngorongoro.

Fei Toto afunguka maisha ya Azam FC
Jeshi la Polisi launga juhudi za Rais kuutangaza utalii