Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi – CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu amewataka Wanachama wa CCM kudumisha umoja na mshikamano, ili chama kiendelee kushinda katika chaguzi mbalimbali ikiwemo ule wa 2024/2025.

Mtemvu ameyasema hayo katika hafla fupi ya kukabidhi Kofia ngumu na viakisi mwanga kwa Madereva Bodaboda Tawi la Bwawani Kata ya Kijitonyama, Wilayani Kinondoni iliyoendana na zoezi la kuwapokea wanachama wapya wa CCM.

Amesema, CCM Mkoa wa Dar es salaam imepokea kadi zaidi ya elfu 20 ili kuwakabidhi Wanachama hao wakati wanasubiri awamu nyingine ya kupokea kadi hizo, ambazo zinaendelea kuboreshwa na Makao Makuu ya CCM.

Kuhusu makundi ndani ya Chama, amewataka wana-CCM kuwaacha Viongozi waliopo madarakani wafanye kazi zao hadi muda wao utapomalizika, ndipo wengine wajitokeze ila kwa sasa kuwaingilia waliopo ni kuwaondoa katika reli na mipango ya kuwatumikia na kuanza kujibu mapigo wakati maendeleo yanasimama.

Polisi watoa onyo kesi za kubambikiana, kukomoana
Zimamoto, WMA waelimisha jamii ujazo Mitungi ya Gesi